Somo la 43: Crypto Exchange ni Nini? Kama umesoma masomo yaliyopita kutoka kwenye “Bitcoin Wallets”, umejifunza Bitcoin wallet ni nini, jinsi ya kuiweka tayari, na jinsi ya kutuma na kupokea Bitcoin. Lakini kama huna Bitcoin yoyote, utaipataje? Utanunuaje Bitcoin? Ili kununua Bitcoin, utahitaji kufungua account kwenye “crypto exchange.” Crypto exchange ni sehemu ambayo wanunuzi na wauzaji wanaweza kufanya trading ya crypto. Crypto exchange hukupa trading platform, mara nyingi ikiwa katika mfumo wa website au mobile app, ambapo unaweza kununua na kuuza crypto. Crypto exchanges pia zinajulikana kama Crypto Asset Trading Platforms (CTPs). Kabla ya kuwepo kwa crypto exchanges, watu waliweza kupata Bitcoin na cryptocurrencies nyingine kupitia mining, au kwa kufanya mazungumzo ya mtu mmoja na mwingine kuhusu transactions kwenye online forums, au hata kufanya transactions ana kwa ana katika maisha halisi. Siku hizi, beginners wengi wa crypto wanaingia kwenye ulimwengu wa crypto kupitia exchange. Makampuni haya yamefanya iwe rahisi kununua Bitcoin haraka kwa kubofya mara chache tu. Kuna exchanges NYINGI SANA zinazofanya kazi, baadhi zikiwa zimeelekezwa zaidi kwa beginners kwenye crypto markets, wakati nyingine zimeundwa kwa ajili ya crypto traders wenye uzoefu zaidi. Exchanges tofauti zina-support cryptocurrencies tofauti, kwa hiyo unaweza kuhitaji kutumia crypto exchanges zaidi ya moja kulingana na kile unachotaka kununua au kuuza. Mwongozo huu utakutambulisha crypto exchanges ni nini na kukusaidia kupata exchange inayokufaa. Crypto exchange ni nini? Crypto exchanges ni websites na apps ambazo unaweza kutumia kubadilisha cryptocurrency moja uliyonayo kwenda cryptocurrency nyingine. Kwa maana maalum zaidi, cryptocurrency exchange ni online trading platform ambayo unaweza kutumia kununua, kuuza na kufanya trading ya cryptocurrencies. Trading platforms hizi zinaitwa “exchange” kwa sababu jukumu lao kubwa ni kuwaunganisha wanunuzi na wauzaji (MATCH buyers and sellers) na si wao wenyewe kuwa sehemu ya transaction. Hata hivyo, hutoza fee kwa kuwezesha kila transaction. Kulingana na crypto exchange, unaweza kutumia traditional fiat currency kama U.S. dollars kununua cryptocurrency. Kwa mfano, unaweza kununua Bitcoin (BTC) kwa U.S. dollars (USD). Au unaweza kutumia cryptocurrencies nyingine. Kwa mfano, kama tayari una Bitcoins, unaweza kununua Litecoin (LTC) kwa kutumia Bitcoins zako (BTC). Kwa kifupi, crypto exchange inakuruhusu: Kununua Bitcoin na cryptocurrencies nyingine Kubadilisha cryptocurrencies ulizonazo kwenda cryptocurrencies nyingine Kuuza cryptocurrencies zako na kutoa pesa Aina tofauti za crypto exchanges ni zipi? Kwa ujumla, neno “exchange” hutumika kuelezea trading platform yoyote inayoruhusu kubadilishana currencies. Lakini kwenye crypto, kuna aina mbili za exchanges: Centralized Crypto Exchanges (CEX) Decentralized Crypto Exchanges (DEX) Lakini ipi ni bora kwa beginners? Hebu tufanye overview fupi ya zote mbili ili kuona ni chaguo gani lina maana zaidi. Centralized Exchange Centralized Crypto Exchange (CEX) kwa kawaida ni biashara ya mtandaoni ambapo users wanaweza kufungua account ili: Kununua/kuuza Kutuma/kupokea Kuhifadhi cryptocurrencies kama Bitcoin (BTC) Hii inafanana sana na forex na stock trading platforms zinazopatikana kwenye traditional finance (“TradFi”). Assets zilizopo kwenye centralized platform ziko chini ya custody ya biashara hiyo. Kwa sababu CEX ina control kubwa juu ya pesa za users, biashara hizi kwa kawaida huwa chini ya regulation kubwa. Kufuata financial regulations za nchi au maeneo wanakofanyia kazi huwapa uwezo wa kuruhusu users kuunganisha bank accounts zao ili kuweka pesa kwenye CEX accounts zao. Decentralized Exchange Decentralized Crypto Exchange (DEX) ni sehemu ambayo crypto traders hufanya transactions moja kwa moja wao kwa wao. Inachukuliwa kama alternative ya traditional centralized exchanges.
Bitcoin Safaris & Education共有
出典:原文を表示
免責事項: 本ページの情報はサードパーティからのものであり、必ずしもKuCoinの見解や意見を反映しているわけではありません。この内容は一般的な情報提供のみを目的として提供されており、いかなる種類の表明や保証もなく、金融または投資助言として解釈されるものでもありません。KuCoinは誤記や脱落、またはこの情報の使用に起因するいかなる結果に対しても責任を負いません。
デジタル資産への投資にはリスクが伴います。商品のリスクとリスク許容度をご自身の財務状況に基づいて慎重に評価してください。詳しくは利用規約およびリスク開示を参照してください。
