source avatarBitcoin Safaris & Education

Chia sẻ

SOMO LA 47: KYC NI NINI? Najua huenda unajiuliza... Hapana. Samahani. Kwa bahati mbaya, KYC si aina mpya ya kuku wa Kentucky! 😂 KYC ni nini? Unapofungua account kwenye crypto exchange, unaweza kugundua kwamba exchange inakutaka ufanye mchakato unaoitwa “KYC verification.” Crypto exchanges nchini Marekani na katika nchi nyingine nyingi zinafuata sheria na kanuni za kupambana na utakatishaji wa pesa (Anti-Money Laundering — AML). Ili kufuata sheria hizi, crypto exchanges zinatakiwa kukusanya taarifa maalum kuhusu wateja wao. Mchakato huu kwa kawaida huitwa KYC, ambao ni kifupi cha “Know Your Customer”, yaani “Mjue Mteja Wako.” Hii ina maana kwamba utatakiwa kutoa taarifa binafsi zinazothibitisha utambulisho wako. Kwa nini KYC inahitajika? Ili kuzuia pesa kutumika kwenye utapeli, utakatishaji wa pesa, kufadhili ugaidi, kujifanya mtu mwingine, au shughuli nyingine haramu, crypto exchanges zinapaswa kufanya ukaguzi zaidi. Kwa kukusanya taarifa kuhusu utambulisho wa wateja wao, database hutengenezwa ambayo vyombo vya sheria vinaweza kutumia katika uchunguzi endapo kutatokea shughuli za uhalifu hapo baadaye. “Know Your Customer” (KYC) si jambo linalohusu crypto pekee. Linatumika pia kwenye karibu taasisi zote za kifedha zinazoshikilia pesa za wateja. Kwa mfano, unapofungua account ya benki, kuomba credit card, mkopo wa gari au mortgage, tayari unapitia mchakato wa KYC. Kuna viwango tofauti vya KYC, kuanzia hakuna KYC kabisa hadi KYC yenye ukaguzi wa kina sana. Ingawa baadhi ya crypto exchanges bado zinaweza kuruhusu watumiaji kuweka pesa bila kupitia KYC, exchanges za aina hii zinazidi kupungua kadiri KYC inavyokuwa kiwango kinachotumika duniani kote. Siku hizi, crypto exchanges nyingi kubwa zinahitaji KYC mara tu mtumiaji mpya anapofungua account. KYC inafanyaje kazi? Unapofungua account kwenye exchange, utatakiwa kutoa taarifa zako za msingi kama vile: - Jina lako kamili - Tarehe yako ya kuzaliwa - Anuani yako - Email address - Namba yako ya simu Taarifa hizi zinahitajika ili kuhakikisha kwamba exchange inatimiza matakwa ya sheria za Anti-Money Laundering (AML). Lengo la sheria za AML ni kuzuia watu kuficha chanzo, mzunguko na mwisho wa pesa zinazotumwa kwa njia ya kielektroniki, ili vyombo vya sheria viweze kufuatilia mzunguko wa pesa zinazotokana na shughuli haramu. Huwezi kujificha ikiwa unatakiwa kuthibitisha utambulisho wako. Kulingana na trading platform au sheria za eneo husika, exchange inaweza pia kukuomba taarifa za ziada kama: - Chanzo cha kipato chako - Namba yako ya Social Security - Kitambulisho chenye picha kilichotolewa na serikali, kama leseni ya udereva au passport - Uthibitisho wa anuani, kama nakala ya bili ya huduma za nyumbani - Picha yako (selfie) - Facial biometric scan, yaani video selfie inayotumika kuthibitisha uso wako Mchakato wa awali wa kujisajili mara nyingi huwa automated, lakini taasisi za kifedha huwa na timu za huduma kwa wateja, yaani watu halisi, wanaokagua tena kama taarifa ulizotoa ni sahihi.

Tuyên bố miễn trừ trách nhiệm: Thông tin trên trang này có thể được lấy từ bên thứ ba và không nhất thiết phản ánh quan điểm hoặc ý kiến của KuCoin. Nội dung này chỉ được cung cấp cho mục đích thông tin chung, không có bất kỳ đại diện hay bảo đảm nào dưới bất kỳ hình thức nào và cũng không được hiểu là lời khuyên tài chính hay đầu tư. KuCoin sẽ không chịu trách nhiệm về bất kỳ sai sót hoặc thiếu sót nào hoặc về bất kỳ kết quả nào phát sinh từ việc sử dụng thông tin này. Việc đầu tư vào tài sản kỹ thuật số có thể tiềm ẩn nhiều rủi ro. Vui lòng đánh giá cẩn thận rủi ro của sản phẩm và khả năng chấp nhận rủi ro của bạn dựa trên hoàn cảnh tài chính của chính bạn. Để biết thêm thông tin, vui lòng tham khảo Điều khoản sử dụngTiết lộ rủi ro của chúng tôi.