SOMO LA 47: KYC ni nini? Unaenda ukiuliza... Hapana. Samahani. Kwa bahati mbaya, KYC si aina mpya ya kuku wa Kentucky! đ KYC ni nini? Unapofungua account kwenye crypto exchange, unaweza kugundua kwamba exchange inakutaka ufanye mchakato unaoitwa âKYC verification.â Crypto exchanges nchini Marekani na katika nchi nyingine nyingi zinafuata sheria na kanuni za kupambana na utakatishaji wa pesa (Anti-Money Laundering â AML). Ili kufuata sheria hizi, crypto exchanges zinatakiwa kukusanya taarifa maalum kuhusu wateja wao. Mchakato huu kwa kawaida huitwa KYC, ambao ni kifupi cha âKnow Your Customerâ, yaani âMjue Mteja Wako.â Hii ina maana kwamba utatakiwa kutoa taarifa binafsi zinazothibitisha utambulisho wako. Kwa nini KYC inahitajika? Ili kuzuia pesa kutumika kwenye utapeli, utakatishaji wa pesa, kufadhili ugaidi, kujifanya mtu mwingine, au shughuli nyingine haramu, crypto exchanges zinapaswa kufanya ukaguzi zaidi. Kwa kukusanya taarifa kuhusu utambulisho wa wateja wao, database hutengenezwa ambayo vyombo vya sheria vinaweza kutumia katika uchunguzi endapo kutatokea shughuli za uhalifu hapo baadaye. âKnow Your Customerâ (KYC) si jambo linalohusu crypto pekee. Linatumika pia kwenye karibu taasisi zote za kifedha zinazoshikilia pesa za wateja. Kwa mfano, unapofungua account ya benki, kuomba credit card, mkopo wa gari au mortgage, tayari unapitia mchakato wa KYC. Kuna viwango tofauti vya KYC, kuanzia hakuna KYC kabisa hadi KYC yenye ukaguzi wa kina sana. Ingawa baadhi ya crypto exchanges bado zinaweza kuruhusu watumiaji kuweka pesa bila kupitia KYC, exchanges za aina hii zinazidi kupungua kadiri KYC inavyokuwa kiwango kinachotumika duniani kote. Siku hizi, crypto exchanges nyingi kubwa zinahitaji KYC mara tu mtumiaji mpya anapofungua account. KYC inafanyaje kazi? Unapofungua account kwenye exchange, utatakiwa kutoa taarifa zako za msingi kama vile: - Jina lako kamili - Tarehe yako ya kuzaliwa - Anuani yako - Email address - Namba yako ya simu Taarifa hizi zinahitajika ili kuhakikisha kwamba exchange inatimiza matakwa ya sheria za Anti-Money Laundering (AML). Lengo la sheria za AML ni kuzuia watu kuficha chanzo, mzunguko na mwisho wa pesa zinazotumwa kwa njia ya kielektroniki, ili vyombo vya sheria viweze kufuatilia mzunguko wa pesa zinazotokana na shughuli haramu. Huwezi kujificha ikiwa unatakiwa kuthibitisha utambulisho wako. Kulingana na trading platform au sheria za eneo husika, exchange inaweza pia kukuomba taarifa za ziada kama: - Chanzo cha kipato chako - Namba yako ya Social Security - Kitambulisho chenye picha kilichotolewa na serikali, kama leseni ya udereva au passport - Uthibitisho wa anuani, kama nakala ya bili ya huduma za nyumbani - Picha yako (selfie) - Facial biometric scan, yaani video selfie inayotumika kuthibitisha uso wako Mchakato wa awali wa kujisajili mara nyingi huwa automated, lakini taasisi za kifedha huwa na timu za huduma kwa wateja, yaani watu halisi, wanaokagua tena kama taarifa ulizotoa ni sahihi.
Bitcoin Safaris & EducationāĻļā§āϝāĻŧāĻžāϰ
āĻā§āϏ:āĻāϏāϞ āĻĻā§āĻāĻžāύ
āĻĻāĻžāĻŦāĻŋāϤā§āϝāĻžāĻ: āĻāĻ āĻĒā§āώā§āĻ āĻžāϰ āϤāĻĨā§āϝ āϤā§āϤā§āϝāĻŧ āĻĒāĻā§āώā§āϰ āĻāĻžāĻ āĻĨā§āĻā§ āĻĒā§āϰāĻžāĻĒā§āϤ āĻšāϤ⧠āĻĒāĻžāϰ⧠āĻāĻŦāĻ āĻ
āĻāϤā§āϝāĻž KuCoin āĻāϰ āĻŽāϤāĻžāĻŽāϤ āĻŦāĻž āĻŽāϤāĻžāĻŽāϤ āĻĒā§āϰāϤāĻŋāĻĢāϞāĻŋāϤ āĻāϰ⧠āύāĻžāĨ¤ āĻāĻ āĻŦāĻŋāώāϝāĻŧāĻŦāϏā§āϤ⧠āĻļā§āϧā§āĻŽāĻžāϤā§āϰ āϏāĻžāϧāĻžāϰāĻŖ āϤāĻĨā§āϝāĻāϤ āĻāĻĻā§āĻĻā§āĻļā§āϝ⧠āĻĒā§āϰāĻĻāĻžāύ āĻāϰāĻž āĻšāϝāĻŧ, āĻā§āύ āϧāϰāύā§āϰ āĻĒā§āϰāϤāĻŋāύāĻŋāϧāĻŋāϤā§āĻŦ āĻŦāĻž āĻāϝāĻŧāĻžāϰā§āύā§āĻāĻŋ āĻāĻžāĻĄāĻŧāĻžāĻ, āĻŦāĻž āĻāĻāĻŋāĻā§ āĻāϰā§āĻĨāĻŋāĻ āĻŦāĻž āĻŦāĻŋāύāĻŋāϝāĻŧā§āĻ āĻĒāϰāĻžāĻŽāϰā§āĻļ āĻšāĻŋāϏāĻžāĻŦā§ āĻŦā§āĻāĻžāύ⧠āĻšāĻŦā§ āύāĻžāĨ¤ KuCoin āĻā§āύ⧠āϤā§āϰā§āĻāĻŋ āĻŦāĻž āĻŦāĻžāĻĻ āĻĒāĻĄāĻŧāĻžāϰ āĻāύā§āϝ āĻŦāĻž āĻāĻ āϤāĻĨā§āϝ āĻŦā§āϝāĻŦāĻšāĻžāϰā§āϰ āĻĢāϞ⧠āϝ⧠āĻā§āύ⧠āĻĢāϞāĻžāĻĢāϞā§āϰ āĻāύā§āϝ āĻĻāĻžāϝāĻŧā§ āĻĨāĻžāĻāĻŦā§ āύāĻžāĨ¤
āĻĄāĻŋāĻāĻŋāĻāĻžāϞ āϏāĻŽā§āĻĒāĻĻā§ āĻŦāĻŋāύāĻŋāϝāĻŧā§āĻ āĻā§āĻāĻāĻŋāĻĒā§āϰā§āĻŖ āĻšāϤ⧠āĻĒāĻžāϰā§āĨ¤ āĻāĻĒāύāĻžāϰ āύāĻŋāĻā§āϰ āĻāϰā§āĻĨāĻŋāĻ āĻĒāϰāĻŋāϏā§āĻĨāĻŋāϤāĻŋāϰ āĻāĻĒāϰ āĻāĻŋāϤā§āϤāĻŋ āĻāϰ⧠āĻāĻāĻāĻŋ āĻĒāĻŖā§āϝā§āϰ āĻā§āĻāĻāĻŋ āĻāĻŦāĻ āĻāĻĒāύāĻžāϰ āĻā§āĻāĻāĻŋ āϏāĻšāύāĻļā§āϞāϤāĻž āϏāĻžāĻŦāϧāĻžāύ⧠āĻŽā§āϞā§āϝāĻžāϝāĻŧāύ āĻāϰā§āύāĨ¤ āĻāϰāĻ āϤāĻĨā§āϝā§āϰ āĻāύā§āϝ, āĻ
āύā§āĻā§āϰāĻš āĻāϰ⧠āĻāĻŽāĻžāĻĻā§āϰ āĻŦā§āϝāĻŦāĻšāĻžāϰā§āϰ āĻļāϰā§āϤāĻžāĻŦāϞ⧠āĻāĻŦāĻ āĻā§āĻāĻāĻŋ āĻĒā§āϰāĻāĻžāĻļ āĻĒāĻĄāĻŧā§āύāĨ¤